Kwa mujibu wa mpango huo, umri wa kustaafu nchini Ufaransa umeongezeka kutoka miaka 62 hadi 62. Marekebisho hayo ya umri wa wastaafu yamepingwa vikali na vyama vya wafanyakazi.
Baada ya vuta nikuvute ya miezi kadhaa iliyoshuhudia maandamano ya kupinga mpango huo, hatimaye Rais wa Ufaransa amesaini muswada huo na kuwa sheria.
Serikali ya Rais Macron imekataa kulegeza kamba na imeendelea kushikilia uamuzi wake wa kuongeza umri wa kustaafu ikitaka kutekelezwa haraka mpango huo wenye utata uliokabiliwa na upinzani mkubwa wa umma.
Mlolongo wa maandamano yan miezi kadhaa nchini Ufaransa umeiweka serikali ya Macron katika mashinikizo makubwa sambamba na migomo katika baadhi ya sekta ambazo zimekuwa zikiungana na waandamanaji.
Mpango wa kuongeza umri wa kustaafu ulikuwa gumzo na mjadala pia mwaka 2019 na katika mwaka huo ulikabiliwa na upinzani mkali pia.
Jumuiya za Wafanyakazi nchini Ufaransa zimetangaza mara chungu nzima upinzani wake dhidi ya mpango huo.
Badhi ya wajuzi wa mambo wanaamini kuwa, hali ya mambo hapo baadaye nchini Ufaransa itazidi kuwa mbaya hasa baada ya mpango wa kuongeza umri wa kustaafu kupasishwa lichha ya kupingwa vikali. Hii ni kwa sababu tayari wananchi wa nchi hiyo wanataabika kutokana na mlolongo wa mambo ambayo umeyafanya maisha katika nchi hiyo ya bara Ulaya kuwa magumu.
342/